|
A Closer Walk - Volume 1 Archive |
|
English Message | Spanish Message |
|
Dhamiria Kubadilika |
|
|
| Je, tutafanya nini tofauti mwaka huu? Kuna maazimio mengi yaliyowekwa juma la kwanza la Januari kuliko wakati wowote wa mwaka- lisho bora linaanzishwa na majaribu mengi kwa kila hali ili kujiimarisha kibinafsi. Ninakiri niliazimia kukimbia maili elfu moja mwaka huu. Nitakiri pia kwamba sijapiga hatua kubwa kutoka pa kwanzia-Nimekimbia maili mbili pekee kwa siku za kwanza tano.( Kumbuka: ujumbe huu uliandikwa tarehe 6 Januari , 2003. Nilikimbia maili 1508 mwaka 2003-Mungu asifiwe!!) |
|
| Haijalishi ujumbe huu unasomwa lini, ila leo ni mwanzo wa mwaka mpya. Azimio nyingi zenye nia njema zitasahaulika punde, bali zingine zitaweka mabadiliko mema ya kudumu. Ikiwa itagharimu ahadi ya azimio ya “mwaka mpya” ni kukomesha mazoea mabaya, kurejesha uhusiano uliovunjika au kuimarisha afya yako, basi kwa vyovyote vile kusudia! |
|
| Lakini tunapoangazia ya kale na kwa juhudi kupanga yajayo, wacha tukaelekeza bidii yetu kwa mabadiliko yenye faida ya milele. Yesu alisema dhahiri alipowakemea mafarisayo : kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyanganyi na kutokuwa na kiasi. Safisha kwanza ndani ----- ile nje yake nayo ipate kuwa safi (Mathayo 23:25-26). |
|
| Biblia yanena juu ya ubadili wa kwanza unaotokea tunapofanyika (Viumbe vipya) katika Kristo. Inanena pia juu ya mageuzo yanayoendelea tunapojongea karibu na Mungu na kupata amani na ridhaa ipatikanayo tu kea uwepo wake |
|
| Warumi 12:2 |
| “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Kufanywa upya nia zetu geuza la ndani ambapo “ tunafananishwa na mfano wa mwana wake (Warumi 8:29). |
|
| Ni hali ya kugeuza fikira, umuhimu, na madhumuni yaingiane na ya kristo. “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya kristo Yeso” Wafipi 2:5 KJV). Nia ya Kristo ilikuwa safi, iliyoelekezwa kwa baba, na kunuia kufanya mapenzi yake; “Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimaliza kazi yake” (Yohana 4:34). |
|
| Katika orodha ya vitu ambavyo tutafanya tofauti mwaka ujao, ninaomba tutatenge muda zaida na Mungu katika maombi, muda zaidi kwa Neno Lake, na muda zaidi kumpenda Yeye kwa moyo wetu wote, tukitafuta uwepo Wake, na kwa juhudi kutamani kujua, na kufanya, mapenzi Yake. Na maombi ya kila mmoja wetu kujongea karibu sana na Baba yetu wa Mbinguni na kuona upendo wake ulio mpya na wa kisasa kila siku. Katika mwaka huu mpya, wacha tukadhamirie maazimio ya kudumu tunapodhamiria mageuzo. |
|
| Kuwa Na Siku Njema! |
|
| Steve Troxel |
| God's Daily Word Ministries |